Wednesday, October 21, 2009

SOMO LA SITA (VYAKULA NA MAPISHI)

Baada ya somo hili ni lazima:

(1) Ufahamu kuagiza chakula katika mahoteli na mikahawa utakapotembelea Afrika Mashariki

(2) Kutoa maelekezo na kupika angalau chakula kimoja cha Afrika Mashariki

=> Soma maelezo ya jinsi ya kupika pilau (uk. 103). Fanya zoezi linalofuatia.

=> Chagua chakula kimoja cha Kimarekani au Kiafrika na uelezee mahitaji na hatua za kufuata wakati wa kukiandaaa.

=> Fanya zoezi la Kumi na moja (Zoezi la Kusoma na Kuandika uk 104-105).

Methali: Pilipili usiyoila, yakuwashia nini?

Kitanza ulimi: (1) Wali wa liwali huliwa na wanawali, wasio wanawali hawali wali
(2) Waacheni wali wale wale wali wao

2 comments:

Iannelli said...

Kila wikiendi ninapika sufuria kubwa ya maharagwe. Ungependa kupika maharagwe?

1)Kwanza uoshe maharagwe na pia ushague majiwe madogo yote.
2)Katakata vitunguu na vitunguu saumu. Halafu, kaanga hivi katika mafuta katika sufuria kubwa kama dakika cumi, huchoma!
3)Ongeza maharagwe ambayo umeosha katika sufuria kwa vitunguu. Ongeza maji kulingana na kiwango za marahagwe unaopika. Pia ongeza viungu kama poda ya pilipili na viungu amavyo unapenda.
4)Kisha funika maharagwe kwa muda wa kama masaa mawili, au hadi maharagwe ni yanalaini. Pengine ni lazima uongeze maji yenye sufuria yako, uone hii.
5)Halafu, ongeza nyanya kikombe kimoja, viungu sana, na chumvi sana sana na upike kwa dakika ishirini na thelathini.
6)Ukule maharagwe kwa wali na sosa ya pilipili...chakula kitamu sana!

Iannelli said...

Zoez i la nane: Zoezi la kuandika (Rachel I.)
1) Vitu gani muhimu ambavyo nitahitaji ikiwa ninataka kupika pilau ni nyama, mafuta, maji, vitunguu, tqangawizi, viungo,mchele, sufuria, na moto
2) Pilau huchuka nusu saa kupika, lakini pengine nusu saa mwingine kukatakata mboga na kuosha mchele.
3) Ninaanza kuchemsha maji kwanza.
4) Ongeza=add, katika=in, kama=like, sufuria=pot/pan
5) Ndiyo, kuna tofauti baina ya wali na pilau. Pilau ni yenye vitu vingi kama nyama na vitunguu, n.k. Wali ni yenye chumvi pekee.