Sunday, October 30, 2011

MASOMO YA NDOTO YA AMERIKA

SURA YA KWANZA (Ijumaa wiki ya 10)

I. Wahusika wakuu: Andika maelezo mafupi kuhusu wahusika hawa kwa kutumia maneno yako mwenyewe

1. Isaya Yano aka Isa

2. Namasake Madoa aka “Ndiyo Alaa”

3. Mwamba

4. Mzee Zakayo Wekesa

II. Kuna sarufi yo yote ngumu? Ipi?

III. Andika ufupisho wa sura ya kwanza kwa kutumia maneno yako mwenyewe.

SURA YA PILI (Wiki ya 11)

1.
Kwa nini Isa yuko msituni?

2. Simulia ndoto ya Amerika ya Isa kwa maneno yako mwenyewe.

3. Je, ndoto hiyo ni ya kweli?

4. Kama ndoto ya Issa inavyoonyesha, watu wengi hufikiri kwamba maisha ya Amerika ni maisha ya raha mustarehe. Sasa rafiki yako mliyekutana naye Afrika anakutaka umsaidie kuja Marekani. Yeye anafikiri kwamba akija Marekani atapata maisha mazuri sana - kazi nzuri, pesa nyingi, magari ghali na raha nyinginezo. Mwandikie barua ukimweleza ukweli kuhusu maisha ya Marekani na ungetaka afanye nini. Yeye sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Yeye anasomea ualimu.

5. Andika ufupisho wa sura ya pili kwa maneno yako mwenyewe.

SURA YA TATU (Wiki ya 12)

1. Tunajua ni kwa nini Issa yuko mstuni. Kwa kwa nini Madoa naye yuko mstuni? (uk. 22-23)

2. Eleza jinsi Issa na Madoa wanavyopanga kufika Nairobi.

3. Walipataje pesa za nauli kwenda Nairobi? Walikwenda kwa Mzee Wekesa kufanya nini? (uk. 25-27)

4. Mjadala - wewe una maoni gani kuhusu kuiba? Ni vizuri ama vibaya?

5. Unaweza kuisimulia sura ya tatu nzima kwa rafiki yako? (ufupisho)

6. Kuna sarufi yo yote ngumu katika sura hii?

SURA YA NNE (Wiki ya 13)

1. Katika sura ya nne, Issa na Madoa wanasafiri kwenda wapi? Eleza safari yao kwa ufupi safari yao

2. Eleza mandhari ya Nairobi. Je inafanana na miji ya Marekani.

3. Elezea mandhari ya hoteli ya soko la Burma. Umeipenda hoteli hiyo? Kwa nini?

4. Jina jipya la Madoa ni lipi? Unafikiri ni kwa nini ana jina hilo?

5. Elezea kuhusu Mwamba kwa kirefu. Katika sura ya kwanza mlisema kwamba mnampenda. Je bado mnampenda Mwamba? (uk. 31-35). Unafikiri Mwamba anafanya kazi gani?

6. Mwamba na Madoa walikwenda kufanya kazi gani Buruburu? (uk 34)

7. Ielezee ndoto ya pili ya Madoa (uk.35 )

8. Andika ufupisho wa sura nzima ya nne. Kuna sarufi yo yote ngumu?

SURA YA TANO (Wiki ya 14)

1. Katika sura ya tano, Issa, Mwamba na Madoa wanapelekwa jela. Kwa nini?

2. Jina halisi la Mwamba ni nani?

3. Soma ukurasa wa 40 - 41 na eleza Mwamba hasa ni nani.

4. Madoa anashtakiwa kwa makosa gani? Na Issa je? Soma maelezo ya Issa chini ya ukurasa wa 43 na mwanzo wa ukurasa wa 44.

5. Simulia mambo yanayotokea katika sura ya tano kwa kutumia maneno yako mwenyewe.

6. Kuna sarufi yo yote ngumu?


SURA YA SITA (Wiki ya 15) 1. Nini kinatokea katika sura ya sita? Mwamba yuko wapi? 2. Andika ufupisho wa sura yote. 3. Umeipenda hadithi hii fupi? Kwa nini?

Wednesday, October 26, 2011

Chakula Nikipendacho

Chakula nikipendacho ni nyama ya n'gombe na mchicha. - Na Robert

Ili kupika chakula hiki kuwatosha watu wawilli, ni lazima kuwa na :

Siagi vijiko viwilli
Mchicha poundi robo
Chumvi ya kutosha
Nyama ya n'gombe paundi moja
Viungo vinavyoitwa "Montreal Steak Spice"

Kinavyopikwa:
Weka viungo katika nyama

Pika nyama ya n'gombe katika grill kwa dakika kumi au hadi ni nyekundu. (Usikipenda nyama nyekunda, upike kwa muda zaidi)

Baada ya nyama ilipikwa, weka mchicha katika sufuria kubwa.
Weka vijiko villi cha siagi katika mchicha . Halafu chumvi.
Pika mchicha kwa dakika tano, ukichanganya.

MAPISHI YA VYAKULA MBALIMBALI (RECIPES): KEKI YA MATUNDA (NA CECILIA)

Mahitaji

Unga wa mahindi vikombe 1 1/3
unga wa ngano kikombe 2/3
sukari kikombe 1 1/4
vanilla kijiko kimoja
mala nusu kikombe
mayai manne
siagi kikombe 3/4
chumvi kijiko
baking powder nusu kijiko
matunda

Upikaji

1. Changanya unga wa mahindi, unga wa ngano, chumvi, na baking powder.
2. Katika bakuli nyingine, changanya sukari, siagi, mayai, vanilla, na mala.
3. Ongeza mchanganyiko wa sukari na mchanganyiko wa unga, na changanya.
4. Ongeza matunda.
5. Pika dakika hamsini kwa 350 digri.
6. Baada ya kupoa, wape watu wale