Friday, September 11, 2009

LEO NI TAREHE 11/9/2009

=> Ulikuwa wapi siku tarehe 11/9/2001? Unakumbuka nini?

=> Ungekuwa rais wa Marekani wakati ule ungefanya nini? Ungeenda kupigana vita Afghanistan na Iraq?

MAZOEZI YA -NGE-, -NGALI- NA -NGELI-

Tazama picha zifuatazo na chini yake uandike mambo ambayo ungefanya na yale ambayo usingefanya kama ungekuwa wewe.

(1) Barack Obama -Raisi wa arobaini na nne wa Marekani













(2) Rush Limbaugh - Mtangazaji wa redio ya kihafidhina



















(3) Machen - Rais wa chuo Kikuu cha Florida



















(4) George Bush - Rais wa arobaini na tatu wa Marekani



















(5) Wewe - kuna kitu cho chote ambacho unafikiri kwamba ni afadhali usingekifanya?

UNAWAPENDA WALIMU?

Walimu ni watu muhimu sana katika maisha yetu. Wao hutufundisha kusoma, kuandika na kuwa na adabu nzuri. Lakini mara nyingi hawalipwi pesa nyingi, wanadharauliwa na wanafanya kazi katika mazingira magumu sana hasa kule Afrika.

Ungekuwa rais wa Tanzania, ungefanya nini kuwasaidia walimu kama huyu pichani anayemfundisha mtoto mdogo kuandika namba tano?

USAFIRI WA HATARI AU?

Watoto hawa ni lazima waende shule na baba ana pikipiki moja tu na hana gari. Je, ungekuwa wewe ungefanya nini?


WATOTO WANAOFANYISHWA KAZI BADALA YA KWENDA SHULE

Una maoni gani kuhusu watoto wadogo kufanyishwa kazi ngumu badala ya kwenda shule?