Tuesday, February 24, 2009

KUHUSU MTIHANI WA KATIKATI - TAFADHALI SOMENI

Mtihani wa katikati utafanyika darasani siku ya Jumanne tarehe 26/2/2009. Mtihani utachukua saa moja na nusu. Topiki/mada za muhimu kuzingatia:

(1) Ni lazima uwe tayari kuandika insha fupifupi juu ya topiki zote ambazo tayari tumeshazisoma darasani mfano; kujistarehesha (somo la 8), Usafiri (somo la tisa), Kuwalea watoto (somo la 10), Hali ya Hewa (somo la 11) na kazi (somo la 12 - alama za ziada).

Kwa hivyo;

=> Utaulizwa maswali mafupi mfano - wewe unajistareheshaje? na utaandika insha fupi. Wewe sasa ni wmanafunzi wa mwaka wa pili na tunakutegemea kwamba unaweza kuandika insha nzuri na kujieleza kwa Kiswahili bila wasiwasi wo wote.

(2) Sarufi: Ni lazima ufahamu hu- tense negative, jinsi ya kufanya contractions, causative (sh-), conditional -ki- (positive na negative) na sarufi yote ambayo umeshasoma mpaka wakati huu. SITAKI ufanye makosa mabaya kabisa ya kisarufi kama vijana VYA, mji ya, mpenzi ya...Makosa kama haya yatakufanya upoteze pointi nyingi sana!

(3) Msamiati: Ni lazima ufahamu maneno yote kutoka zoezi la kusoma la somo la nane (Ninapenda sana kwenda ufukoni - uk 127-128) na zoezi la kusoma la somo la 10 (Malezi yangu - uk 151-152). Utaulizwa kuoanisha maneno (matching), kutafsiri pamoja na kutumia maneno hayo katika sentesi. Unaweza pia kuulizwa kutafsiri msamiati wo wote ambao tumeshaona darasani.

Huu utakuwa ni mtihani rahisi na hakuna shida ya kuwa na wasiwasi. Nitakuwa ofisini mwangu kesho Jumatano (25/2/2009) kuanzia saa sita mchana mpaka saa saba na nusu mchana. Unaweza kufika wakati huo kama una swali lolote. Unaweza pia kuniandikia e-mail kupitia profesamatondo@gmail.com. Nitakuwa nikitazama e-maili hii mara kwa mara.

Asanteni sana!
==================

Thursday, February 12, 2009

CHEMSHABONGO NAMBA TATU - SPRING 2009

(1) Usikilize tena wimbo wa Mtoto Akililia Wembe kutoka you tube aua hapa. Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja kuhusu swali lifuatalo '...mtoto akililia wembe tumpe?" Tumia causative angalau (at least) tano. (alama 20. Ninataka insha ndefu nzuri)

(2) Wewe ukiwa na watoto siku moja, utawapa adhabu gani ili kuwaadabisha? Utawapiga? Kwa nini? Andika jibu refu kuhusu suala hili. (alama 10)

(3) Fanya zoezi la tatu (ukurasa wa 154) katika kitabu chako. Kabla hujajibu swali hili, ni lazima kwanza utembelee hapa. (alama 13)

(4) Je, katika sikukuu hii ya Wapendanao utafanya nini? Andika insha fupi. (alama 10)

MUHIMU: Majibu ya swali la pili ni lazima yawekwe hapa kama maoni (comments). Majibu ya Maswali ya 1, 3 na 4 yaletwe darasani Jumanne ya wiki kesho (17/2/2009)