Wednesday, October 7, 2009

MUME BWEGE (NA BUSHOKE - MWANAMUZIKI WA BONGO FLEVA KUTOKA TANZANIA)



Tazama video hii na soma maneno ya wimbo (lyrics)












MUME BWEGE (NA BUSHOKE – TANZANIA)

Maneno yamewekwa hapa na darasa la Kiswahili la mwaka wa pili

Chuo Kikuu cha Florida, Gainesville


Nilikuwa na mpenzi wangu

Nani asiyemjua

Mtoto kaumbika

Utasema malaika

Miezi kadhaa ikasogea

Mtoto (wa) kwanza tukazaa

Mtoto katoka Mwarabu

Swali lilikosa jibu

Akasema we hujui

Mtoto kafata kwa babu

Nikagunaguna pale mzee nikauchuna


Mtoto (wa) pili tukazaa

Huyu wa sasa Mchina doh

Nikasema mama vipi

Mbona mi sielewi

Akasema we hujui

Huyu kafata kwa bibi


Aa wewe mama wee

Ingekuwa ungefanyeje


Mwenzenu nalala chini

Mke wangu kitandani

Nikilala kitandani

Kila mtu shuka lake

Mwenzenu nalala chini

Mke wangu kitandani

Nikilala kitandani

Basi ujue mzungu wa nne


Nikiuliza kwa nini

Anasema amenipa likizo eeh

Siyo kama napenda

Imenilazimu ooh

Siyo kama napenda

Ananilazimisha yoo


Mwenzenu naosha vyombo

Mwenzenu napiga deki

Mzee mzima napika

Jamani nafua nguo

Siyo kama napenda

Nalazimishwa mimi


Lo, hii sasa kali

Jana kaniambia anataka kwenda klabu na marafiki zake

Ila kaniambia mimi

Nilinde nyumba eti wezi wasije wakaiba

Eee Bize Man hii halali kweli

Oyaa Mbiye njoo unisaidie huku nyumbani mwenziyo naonewa

Chifu Rumanyika, unajifanya hujui

Ooo naonewa mimi

Aa wewe mama wee

Ingekuwa ungefanyeje


MSAMIATI


-jua - fahamu

umbika - naturally attractive

mzungu wa nne - opposite direction

likizo - mapumziko

lazimu - ni lazima

lazimisha - force to do something

osha - wash

vyombo - dishes

piga deki - kusafisha sakafu

fua nguo - wash clothes

linda - protect

wezi - wingi wa mwizi

iba - steal

halali - fair

onea - mistreat

=======================================

MASWALI:

Baada ya kutazama video hii na kusoma maneno ya wimbo huu:


(1) Andika tofauti za kitamaduni kati ya wanaume wa Kitanzania na wanaume wa Kimarekani. Ni lazima utumie kauli ya kutendea (prepositional form) mf. pika - pikia, soma - somea n.k.

Mfano: Kwa kawaida wanaume wa Kitanzania hawajipikii chakula lakini wanaume wa Kimarekani wakati mwingine wanajipikia chakula chao

(2) (Kwa wavulana/wanaume au jifanye (pretend) kuwa mwanaume), kama wewe ungekuwa ndiye unayeimbwa katika wimbo huu ungefanya nini?

(3) Umeupenda wimbo huu? Kwa nini?

5 comments:

Anonymous said...

Video hii inachekesha kwa sababu ndugu za wanaume na wanawake wanachekesha. Kwa kawaida, katika Marekani, wanaume ni watu wabaya ambao ni wazinzi. Lakini katika video, inaonekana wanawake ni wazinzi na wanaume ni wateswa. Ninafikiri ni lazima mume amwache mkewe baada ya mtoto wa kwanza kuzaliwa. Mtu ye yote ambaye haondoki kwa mpenzi wake ambaye ni mzinzi ni bozibozi au bwege. Ninamhurumia mwanaume katika wimbo huu.
-Joy

Anonymous said...

Ninapenda video hii, lakini ninafikiri muziki si kifano kama maneno ya shairi. Maneno yanahuzunika lakini muziki ni furaha sana na mwimbaji anacheza dansi. Ninamwonea huruma kwa sababu mke wake hakuamini- ni kitu kibaya sana. Lakini, simwonea huruma kwa sababu ni lazima asafishe na anajipikia. Ninasafisha na ninajipikia kila siku- si kazi gumu!

Anonymous said...

Video hii inanichekesha pia, kwa sababu mwimbaji anacheza dansi na anachekelea. Anaonekana kujisikia furaha, lakini anaimba kuhusu mpenzi wake kumwonea. Ningesikia huzuni, na ningemwacha mpenzi wangu.
Katika darasa langu la Anthropologia, tulijifunza kuhusu mgawanyo wa kazi Afrika. Wimbo huu unavihakikisha vitu ambavyo nimesoma - kwa kawaida, wanawake wanafanya kazi zaidi.
-Kelley

Anonymous said...

Video hii inanichekesha pia, lakini sipendi dhana ambayo wanaume wanakuwa wakali. Ni dhana yenye makosa. Wake wasiwasafishie wanaume. Ninapenda wanasheria wanawake wanaosaidia wanawake. Kujisafishia kusiwe kubaya.

Anonymous said...

Hii nyimbo ilitoka mwaka gani