Wednesday, September 17, 2008

MASHAMBULIZI YA BOMU YEMEN (MADA YA HUGH)

Jana magaidi waliushambulia ubalozi wa Marekani nchini Yemen kwa bomu la gari na watu zaidi ya kumi wamefariki. Inasemekana magaidi wa Islamic Jihad au Al Qaida ndiyo wamefanya shambulizi hilo. Katika kufanya shambulizi hilo, magaidi walijifanya kuwa polisi wa Yemen. Rais George Bush wa Marekani amesema Marekani haitatishwa na magaidi na aliwaita kuwa ni waoga.
===============
Sasa jaribu kujibu maswali haya:

(1) Magaidi ni watu gani? Wewe unawapenda? Kwa nini?


(2) Wewe ungekuwa rais wa Marekani ungefanya nini kupambana na
magaidi na ugaidi?


(3) Toa maana za maneno yafuatayo:

Wanamgambo, ubalozi

(4) Kuna tofauti gani kati ya kufa na kufariki?


(5) Kujifanya ni nini? Wakati wa Haloween wewe hupenda kujifanya kuwa nani?

1 comment:

Emusaint said...

Wakati wa Haloween mimi hupenda kujifanya kuwa shetani. Mimi ni shetani mzuri. Ningekuwa raisi wa Marekani ningekuwa ningeendelea kupigana, na pia ningesaidia zaidi na maendeleo na ulinzi wa dunia.
-Hugh