Wednesday, April 7, 2010

SHIDA - SURA YA TANO na SITA

Sura ya Tano - Maswali ya Majadiliano


Ijumaa (9/4/2010)

  • Katika sura hii, Sefu yuko wapi? (Nila)
  • Shida alikutanaje tena na wazazi wake (uk 69 – 71)? (Nikki)
  • Sefu na Shida wameamua kurudi kijijini. Kwa nini? Isome vizuri barua ya Sefu aliyomwandikia abake (uk79 – 81) (Gloria na Dkt. Cheka)
  • Tazama tazama matarajio ya maisha bora kule vijijini (aya ya mwisho ukurasa wa 81 – 82). Ni kweli? (Jelani)
  • Sema kidogo juu ya ufupisho wa sura ya tano kwa maneno yako mwenyewe (Renee).


Sura ya Sita - Maswali ya Majadiliano


Wiki ijayo (Jumatatu na Jumatano)


  • Je, umeipenda riwaya ya Shida? Kwa nini? (Andrea)
  • Waswahili wana methali nyingi. Methali moja inasema kwamba “mchagua jembe si mkulima” . Je, unawezaje kutumia methali hii kueleza matatizo ya (Chonya) Sefu kama tulivyoona katika sura ya kwanza mpaka sura ya tatu ya riwaya ya SHIDA? (Safina)
  • Wahusika wakuu wa riwaya hii ni nani? Eleza machache juu ya tabia zao kwa kifupi. Ni yupi ambaye umempenda sana? Kwa nini? (Elena)
  • Eleza maisha ya Matika (Shida)? Je, yeye ni mfano halisi wa hali ya maisha ya wanawake wa Afrika? (Nikki)
  • Umejifunza nini kuhusu maisha ya watu katika Tanzania ya miaka ya sabini (na sasa) baada ya kusoma riwaya ya Shida? (Mwalimu)
  • Je, unaonaje kuhusu suluhisho la mwandishi? Je, kurudi vijijini kwa Chonya, Matika na Msafiri ndilo jibu sahihi kwa matatizo ya vijana na watu wengine wasio na kazi kule mijini? (Simba)

No comments: