Sunday, October 30, 2011

MASOMO YA NDOTO YA AMERIKA

SURA YA KWANZA (Ijumaa wiki ya 10)

I. Wahusika wakuu: Andika maelezo mafupi kuhusu wahusika hawa kwa kutumia maneno yako mwenyewe

1. Isaya Yano aka Isa

2. Namasake Madoa aka “Ndiyo Alaa”

3. Mwamba

4. Mzee Zakayo Wekesa

II. Kuna sarufi yo yote ngumu? Ipi?

III. Andika ufupisho wa sura ya kwanza kwa kutumia maneno yako mwenyewe.

SURA YA PILI (Wiki ya 11)

1.
Kwa nini Isa yuko msituni?

2. Simulia ndoto ya Amerika ya Isa kwa maneno yako mwenyewe.

3. Je, ndoto hiyo ni ya kweli?

4. Kama ndoto ya Issa inavyoonyesha, watu wengi hufikiri kwamba maisha ya Amerika ni maisha ya raha mustarehe. Sasa rafiki yako mliyekutana naye Afrika anakutaka umsaidie kuja Marekani. Yeye anafikiri kwamba akija Marekani atapata maisha mazuri sana - kazi nzuri, pesa nyingi, magari ghali na raha nyinginezo. Mwandikie barua ukimweleza ukweli kuhusu maisha ya Marekani na ungetaka afanye nini. Yeye sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Yeye anasomea ualimu.

5. Andika ufupisho wa sura ya pili kwa maneno yako mwenyewe.

SURA YA TATU (Wiki ya 12)

1. Tunajua ni kwa nini Issa yuko mstuni. Kwa kwa nini Madoa naye yuko mstuni? (uk. 22-23)

2. Eleza jinsi Issa na Madoa wanavyopanga kufika Nairobi.

3. Walipataje pesa za nauli kwenda Nairobi? Walikwenda kwa Mzee Wekesa kufanya nini? (uk. 25-27)

4. Mjadala - wewe una maoni gani kuhusu kuiba? Ni vizuri ama vibaya?

5. Unaweza kuisimulia sura ya tatu nzima kwa rafiki yako? (ufupisho)

6. Kuna sarufi yo yote ngumu katika sura hii?

SURA YA NNE (Wiki ya 13)

1. Katika sura ya nne, Issa na Madoa wanasafiri kwenda wapi? Eleza safari yao kwa ufupi safari yao

2. Eleza mandhari ya Nairobi. Je inafanana na miji ya Marekani.

3. Elezea mandhari ya hoteli ya soko la Burma. Umeipenda hoteli hiyo? Kwa nini?

4. Jina jipya la Madoa ni lipi? Unafikiri ni kwa nini ana jina hilo?

5. Elezea kuhusu Mwamba kwa kirefu. Katika sura ya kwanza mlisema kwamba mnampenda. Je bado mnampenda Mwamba? (uk. 31-35). Unafikiri Mwamba anafanya kazi gani?

6. Mwamba na Madoa walikwenda kufanya kazi gani Buruburu? (uk 34)

7. Ielezee ndoto ya pili ya Madoa (uk.35 )

8. Andika ufupisho wa sura nzima ya nne. Kuna sarufi yo yote ngumu?

SURA YA TANO (Wiki ya 14)

1. Katika sura ya tano, Issa, Mwamba na Madoa wanapelekwa jela. Kwa nini?

2. Jina halisi la Mwamba ni nani?

3. Soma ukurasa wa 40 - 41 na eleza Mwamba hasa ni nani.

4. Madoa anashtakiwa kwa makosa gani? Na Issa je? Soma maelezo ya Issa chini ya ukurasa wa 43 na mwanzo wa ukurasa wa 44.

5. Simulia mambo yanayotokea katika sura ya tano kwa kutumia maneno yako mwenyewe.

6. Kuna sarufi yo yote ngumu?


SURA YA SITA (Wiki ya 15) 1. Nini kinatokea katika sura ya sita? Mwamba yuko wapi? 2. Andika ufupisho wa sura yote. 3. Umeipenda hadithi hii fupi? Kwa nini?

15 comments:

Jelani said...

Sura ya Moja:

I.
Isa ni mtoto mskini lakini ana mama mzuri alimsadia na baba yake kufa. Isa aliisha katika shamba na kijiji wake linaitwa Sangura. Isa anaweza kumsaidia mama yake na shamba lao na alihudhuria shule.

Isa ana rafiki kubwa anaitwa Madoa lakini watu wengi wanamitwa “Ndyio Alaa” kwa sababu yeye husema “ndyio Alla” kila wakati akikuwa akipenda. Jamaa yake wana shamba kubwa kidogo kuliko shamba ya Isa. Madoa hapendi kusoma. Anataka kusafiri Amerika.

Madoa alisema rafiki yake Mwamba alijua lenga nyingi. Madoa angetaka kuwa Mwamba.

Mzee Wakayo Wakesa ana fimbo na alipenda kusema Kishahili kikale. Anafikiri ‘nduku’ yake anakufa.

II.
Kuna maneno makubwa ambao sijui. Lakini kwa kawaida nisingefahamu sarufi nyingine, ningepata wakusi wakuu za hadithi.

III.
Madoa anataka kwenda America. Anapata ndoto ya America sana. Alijaribu kuambia Isa na Isa alimcheka. Kijiji cha Sangura kuna wanaume ambao kufa. Wanawake wanauzaa chakula na vitu vingi katika soko lakini watu wote ni maskini. Nafikiri Madoa atajaribu kuondoka Africa Mashariki tena na tena.

Angela said...

Sura Ya kwanza:
I. Isa ni mtoto anakaa katika shmaba na mama wake. Isa na jamaa waka ni tabaka la chini. Nyumba wao ina mashimoyaliyoko paani. Isa sina furaha kwa sababu anachukia nymba, anachukia kulima shamba, anachukia shule wakati wa kusoma, na vitu vingi.

Madoa, au "Ndiyo Alaa," ni rafiki mkubwa wa Isa. Sina furaha pia. Madoa si mjanaja, ni mjinga kwa sababu hanahudhuria masomo kila siku. Anataka kusafiri "Amerika" kwa sababu anchukia maisha katika kijiji cha Sangura.

Mwamba ni rafiki wa Madoa. Ni mjinga sana na anajua lugha nyingi kwa sababu amesafiri nchi nyingi. Mwamba anataka kusaidia Madoa.

Mzee Zakayo Wekesa ni huzuni. Anakilia machozi nduku yake nakufa. Moyo wake una uchungu.

II. Ninaelewa sarufi sana, lakini vitu vyache sijui. Kwa mfano, mwandishi anatumia sarufi sana:
"Alikuwa anasema" Kuwa + present tense
Ninakumbuka kujifunze sarufi hii, lakini sikunbuki maana. Hadithi ina maneno sijui, lakini ninatafuta maneno katika kamusi. Nilielewa hadithi jumla.

III. Isa na Madoa wanakuwa rafiki makubwa. Wanachukia maisha katika kijiji cha Sangara. Madoa anatana mtu jina lake ni Mwamba. Mwamba anataka kusaidie Isa kusafiri Merekani. Madoa ni msisimko kuenda Merekani na kubahili jina yake. Isa hapendi mipongo ya Madoa na Mwamba. Wanaona Mzee Wekesa na Mzee anakilia machozi.

Jelani said...

Sura ya nna maswali

1. Isa na Madoa walipanda matatu na walisafari Eldoret, Nakuru, Gilgil, Naivasha, na Nairobi. Kondukta alipowatakia pesa, Madoa hakujua kusabu pesa.
2. Nairobi una majengo makubwa na watu wengi sana. Isa uliogopwa Nairobi kwa sababu hakujui mji huo mbele wala nyuma yake.
3. Hoteli ya soko la Burma ilipika matumbo. Nzi wengi walikula pamoja na wageni. Ni chafuchafu. Nimeipenda hoteli kama hoteli ya soko la Burma kwa sababu ni rahisi sana.
4. Madoa anaitwa “Ninja” na Rock Mwamba. Nafikiri ana jina hilo kwa sababu anaiba vitu au anapiga watu na Mwamba.
5. Mwamba ni mweusi sana. Anavaa nguo ghali na rasta na ana sauti kubwa. Sipendi Mwamba kwa sababu alimpa banduki Madoa. Nafikiri Mwamba anafanya kazi na polisi mabaya wa Kenya.
6. Madoa alitaka kufanya kazi alisemwa Mwamba. Hakuhitaji kupumzpika. Isa hakujia kazi gani na aliogopa kuuliza. Lakini Isa anajua usimchezee Mwamba. Mwamba na Madoa tunataka kufanya kazi na bunduki. Nafikiri kazi wao ni mbaya.
7. Katika ndoto ya pili, Isa ni rais wa Amerika, au “Marekani.” Alisema “katika Amerika hakuna walimu wabaya, hakuna umaskini, hakuna watato anayecharazwa viboko.”
8. Sijui “hajanifafanulia” (33) au “nilivyogundua” (31) au “umetufunika” (30).

Jelani said...

"nna" ni nne. samahani.

Anonymous said...

Kayla Stewart
Profesa Matondo
SWA 2200
Tarehe ni ishirini na tisa mwezi wa octoba mwaka elfu mbili na kumi

SURA YA KWANZA
I.Herufi
1) Isaya Yano aka Isa
 hapendi kusoma lakini anaenda shule, na hapendi kulima lakini anapenda kucheza
 anakaa katika nyumba ndogo mwenye mamake na baba wake kufa
 ni yenye halisi (realistic) na ya huruma (sympathetic) na mwepesi (sensitive)
 ni mtoto mwa ajabu (curious)
 ni mhusika (main character)

2) Namasake Madoa aka “Ndiyo Alaa”
 yeye ni kama Isa lakini si ya huruma au mwepesi
 ni anapenda mpoteza wakati (daydream) kuhusu Amerika
 anakaa katika nyumba ndogo lakini kubwa kuliko nyumba ya Isa
 hapendi kusoma sana na kulima lakini anapenda kucheza
 haendi shule na anaenda pahali pengine lakini Isa au watu wengine hajui wapi
 ni mtoto na anafikiri (thinks) kila mtu katika Marekani ana jina Michael kama rais, “Mike Tyson”
 ni mwenye tama ya makuu (ambitious)
 yeye ana fikra (imagination) kubwa

3) Mwamba
 ni mtu ambaye asafiri sana
 anaweza kusema lugha zingi
 ni sanamu (idol) ya Madoa

4) Mzee Zakayo Wekesa
 ni mwalimu na mwepesi
 hawezi kutembea sana na ana henzerani (cane) au fimbo kumsaidia anatembea
 ana mzigo kwa sababu anaenda mazishi (funeral) kwa hivo mzee anapindua (upset)
 hawezi kusema Kiswahili sana kwa sababu yeye alisema ambayo “nduku yangu nakufa” (his antelope is dying)

II. Sarufi
 sio
 pasipojulikana
 nikamgeukia
 inyeshapo
 akinionya
 “zingepita huku akiwa hajulikani aliko”
 Hata liwa liwalo
 Muzuri kitoko

III. Ufupisho
Sura ya kwanza ni kuhusu watoto wapili lakini Isa ni mhusika. Mtoto mwingine ni Madoa naye anataka kwenda Amerika kwa sababu hapendi kwetu kwa hivyo anaota kuhusu ndoto ya Marekani sana. Lakini, yeye hajui Amerika sana. Isa na Madoa hawapendi kwao kwa sababu mama wao wakiwachapa Isa na Madoa wakati wao walipokataa kusaidia kulima mashamba yao. Pia, hawapendi kwao kwa sababu wao ni maskini wenye nyumba ndogo na hawapendi shule sana. Madoa anakusudia (determined to) kwenda Amerika lakini Isa anaona shaka (doubts) Madoa ataweza kwenda Amerika.

Rachel Velez said...

Profesa Matondo
SWA 220
Tarehe saba, mwezi wa novemba, mwaka elfu mbili na kumi

I.
Isa ni mhusika mkuu wa Ndoto ya Amerika mwenye anakaa kijijini cha Sangura katika tarafa ya Cherangani, Wilayani Trans-Nzoia. Babake alikufa alipokuwa bado mdogo sana, basi Isa amekuwa anaishi na mama yake. Wao si matajiri, na wanakaa nyumbani kwamba ina kuta za udongo. Shamba lao ni dogo, pia. Isa hapendi shule, lakini anapenda kucheza, na anampenda rafiki yake mkubwa sana – Madoa, au “Ndiyo Alaa!”

Madoa ni mcheshi sana, na rafiki mkubwa wa Isa. Hapendi shule na hakuwa anahudhuria masomo kwa sababu anatembelea miji mingine mikubwa nichini Kenya. Madoa si hodari, lakini yeye ni pasi sana. Sasa angependa kuenda Amerika kwa sababu hataki kusoma, kukaa katika Sangura, kuchapwa viboko, au kufanya kazi nyumbani.

Madoa na Mwamba walikutana Nairobi. Yeye si mtoto kama Madoa na Isa, na Mwamba alitembea dunia nzima, na aliweza kuzungumza lugha nyingi. Madoa angependa kuwa Mwamba.

Mzee Zakayo Wekesa alibeba fimbo na mzigo mkononi kwa sababu alienda mazishi. Alisikitika sana na alilia machozi, lakini hawezi kusema Kiswahili kizuri basi Madoa alimcheka kwa sababu Mzee Zakayo Wekesa alisema “nduku yangu nakufa.”

II.
- inyeshapo
- pasipovuja
- alijulikana
- nisishirikiane
- itwaye
- ninakudanganya

III.
Sura ya kwanza kuhusu wahusika wapili Isa na rafiki yake Madoa. Isa ni mhusika mkuu wa kitabu hiki, na tulisoma kuhusu jamaa yake na kwamba hapendi kusoma na anachukia kufanya kazi nyumbani. Lakini, Isa ni mpole sana na anamjali Madoa sana. Madoa, au “Ndiyo Alaa”, ni mcheshi lakini si hodari na hajui masomo yake, kwa hivyo haendi shule. Anataka kuenda Marekani kwa sababu anachukia Sangura sana sana. Lakini, Madoa hajui nchi ya Marekani yoyote!

Mary-Alison Burger said...

I.

Isa ni mtoto mdogo, yeye ana rafiki mkubwa, nija lake ni "Madoa" au "Ndiyo Alaa." Isa nimechoshwa na kila kitu. Amerrchoshwa mwalimu wake, amechoshwa na maisha katika sangura. Amechoshwa na masomo. Isa sina furaha kwa maisha wake.

Madoa ambaye watu wengi wanamitwa "ndiyo alaa" ni mtoto mdogo pia. Matajiri, madoa hakuwa akihudhuria masomo mara nyingine na hueda alisema ametoka miji mingine badala darasa. Yeye ni ki pumbavu sana.

Mwamba ni "alikuwa mtu mzima aliyetembea dunia nzima" aliweza kuzungumza lugha nyingi. Madoa angetaka kuwa mwamba.

Mzee zakayo wekesa ni mtu ambaye ana huzuni sana jwa sababu nduku yake nafariki.

II)
Nilikuwa kuchanganyikiwa na kutumia "ki" badala "na"

III)

Hadithi hii ni kuhusu watoto wawili wanafikiri kwamba nchi za amerika zitakuwa bora kuliko kuna maisha katika afrika, lakini hawajui chochote kuhusu amerika basi mawazo yao yote ni makosa yote (si wamarekani wote majia yao ni "michael"

Mary-Alison Burger said...

The tense for the verb "choshwa" should be "a"! not "ni" in the last post! and it should say "jina not nija" Oops!

Mary-Alison Burger said...

1. Kwa nini Isa yuko msituni?
Isa yuko msituni kwa sababu mamake anamchapwa viboko. Anafikiri kwamba Isa amerogwa, kwa sababu anasema ambaye anataka kuwa na ndoto ya amerika

2. Simulia ndoto ya Amerika ya Isa kwa maneno yako mwenyewe.
Isa alikuwa na ndoto ya amerika kuhusu Madoa na Isa walienda yuko “New York.” Ndani ya ndoto Madoa na Isa waliendesha gari kubwa na walikuwa na raha mustarehe. Waliingia katika hoteli kubwa, kwa vinywaji vingine mbali mbali na chakula ambacho kinajipika. Pia. Kama unataka kulala kitanda kitakuwa kuja kwa wewe kama kusema “Kitanda njoo”

3. Je, ndoto hiyo ni ya kweli?
Hapana, watu ambao walitoka nchi ya amerika si wote watajiri. Kweli, wamerikani wengi ni maskini. Kwa mfano, mjini wa New Orleans, jimbo la florida, watu wengi ni maskini sana. Pengine maskini zaidi kuliko waafrika. Ni kweli ambaye baadhi ya watu katika amerika wana magari makubwa, na pesa nyingi, watu zaidi wana

4. Kama ndoto ya Issa inavyoonyesha, watu wengi hufikiri kwamba maisha ya Amerika ni maisha ya raha mustarehe. Sasa rafiki yako mliyekutana naye Afrika anakutaka umsaidie kuja Marekani. Yeye anafikiri kwamba akija Marekani atapata maisha mazuri sana - kazi nzuri, pesa nyingi, magari ghali na raha nyinginezo. Mwandikie barua ukimweleza ukweli kuhusu maisha ya Marekani na ungetaka afanye nini. Yeye sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Yeye anasomea ualimu.
Tulifanya katika darasa.

5. Andika ufupisho wa sura ya pili kwa maneno yako mwenyewe.

Sura ya pili ni kuhusu Isa kukumbia msituni kwa sababu mamake alimchapwa viboko sana kwa sababu alifikiri kwamba amerogwa alipomwambia kwamba hajaota juu ya amerika. Muhimu zaidi ni kwamba, Isa amekuwa na anaota kuhusu amerika.

Robert Shelton said...

1. Isa ni mtoto ambaye hapendi vitu vyengi. Anachukia shule, nyumba yake, na kwake. Babake alikufa wakati Isa alipokuwa kijani sana. Yeye ni maskini na anakaa katika nyumba ya msonge. Mamake na yeye wana pesa kwa sababu mamake anafany kazi soko lakini Isa akumsaidia mamake katika soko basi anchapwa na mamake.

Madoa, au Nidyo Alaa kama anaitwa na watu wengi, ni rafiki mkubwa ya Isa. Yeye ni mwotaji na amekuwa na ndoto ya kusafari katika Marekani kwa sababu anachoshwa na chochote juu ya maisha wangu wa Sangura. Mama ya Isa hapendi Madoa kwa sababu Madoa hakwendi madarasa na anaondoka Sangura kusafiri katika Nairobi na mji mingi wa Kenya.

Mwamba ni mtu ambaye amesafiri dunia nzima. Yeye anaweza kusema lugha nyinge. Kwa mfano, ansema Kiingereza, Kijerumani, Kihindi, Kiarabu, Kimaasai, Kikuyu, na Kiluhya. Mwamba anamsaidia Madoa kufanya mpango kuende Marekani.

Mzee Wekesa ni mzee anasemaye Kiswahili vizuri. Alisikitisha kwa sababu ndugu yake alikufa, lakini yeye aliwaambia watoto katika Kiswahili mbaya.

Ndiyo, kuna sarufi ngumu. Kwa mfano, “tulikuwa tukisoma.” Nilisoma hii kama “tulisoma” lakini sijui ikikuwa sawa.

3. Sura ya kwanza inawaanzisha wahusika wakuu. Inaeleza maisha katika Sangura na kwa nini Isa na Madoa hawapendi kwao. Madoa alimzugumza Isa juu ya kusafiri katika Marekani na anakuwaje na rafiki ambaye alisafiri kila mahali duniani. Mwisho wa sura Mzee Wekesa aliwakutana watoto na alilia kwa sababu ndugu alikufa.

Andrew Miller said...

Wiki II Maswali 1-3
1) Isa yuko msituni kwa sababu mamake alimchapa na Isa kuambia kwa msituni.

2) Kwa muda wa ndoto ya Amerika ya Isaya, Isaya aliota kama yeye na Madoa waliendesha gari kubwa katika mji wa New York. Gurudumu moja lilivunja na wao hawakulikaza. Halafu, walienda hoteli kubwa na kula chakula na kulala.

3) Hapana, ndoto hiyo si ya kweli kwa sababu Madoa alisema walikaa Cairo, lakini Isa alisoma kama walikaa New York.

Robert Shelton said...

Sura ya Pili

1. Isa yuko msituni kwa sababu alikuwa anatoroka kutoka mamake. Mamake alikuwa anamcharaza viboko Isa kwa Isa alikuwa ametembea na Madoa.

2. Madoa alisema, "Mara nyingine nikienda sitarudi tena." Ndoto ya Isa inasimulia kwa maneno haya kwa sababu Isa alisafiri katika Amerika na Madoa na tulikuwa tumeanza maishi mpya.

3. Hapana, ndoto hiyo si ya kweli. Ilikuwa ndoto tu. Isa aliamza msituni na akakumbuka ndoto yake kwanza juu ya Amerika.

4. Maisha ya Amerika si raha mustarehe. Watu wengi hawawezi kutafuta kazi. Ni kali sana kutafuta kazi kwa sababu uchumi wa Amerika ni mbaya kidogo. Watu wingine wanafanya kazi sana kwa pesa kidogo sana. Kwa watu fulani, maishi ya Amerika ni raha mustarehe kwa sababu tu walikuwa wamekuwa na pesa.

5. Isa nilisikitisha kwa sababau hakuwa anaota ndoto ya Amerika kama Madoa. Basi, alikuwa akilia na mamake alifikiri Isa alikuwa na wazimu. Mamake alianza kuchapata viboko Isa kwa sababu Isa alikuwa anamzungumza Madoa. Isa alitoroka na alienda msituni. Msituni, Isa alikuwa akaota ndoto ya Amerika juu ya maishi na Madoa katika Amerika. Mwishowe, Isa aliamza na hakurudi nyumbani.

Andrew said...

Sura ya Pili:

3.Rafiki yangu,
Unataka kuja Marekani kwa nini? Hupendi maisha ya Mkenya? Unafikiri maisha ya Marekani ni rahisi? Mara kwa mara maisha ya Marekani si rahisi, ni ngumu, hasa kwa wageni wa Marekani. Utakaa wapi? Nyumba ni ghali sana na hutaki kukaa barabarani. Je, unafikiri kufanya kazi wapi? Marekani haina kazi nzuri nyinge na ungepata kazi baya, ungefanya kazi ngumu na hakupata pesa nyingi. Rafiki yangu, ninataka kukuona, lakini ni afadhali ukae Mkenya.

Iqra Kamal said...

Sura ya Kwanza:
I. Wahusika wakuu:
1) Isaya Yano au Isa anakaa katika kijiji cha Sangura katika tarafa ya Cherangani. Baba yake alifarikia akiwa bado mdogo sana. Isa na Mama yake wanakaana na wao si matajiri. Anapochukia kwao na anachukia shule pia. Mama yake na mwalimu walikuwa wakimchapa viboko.

2) Madoa au "Ndiyo Alaa" ni rafiki mkubwa wa Isa na ni mcheshi sana. Anakaa na Mama yake katika kijiji Sangura lakini Madoa anapochukia kwake pia. Madoa alikuwa akipenda kusema "Ndiyo Alaa!" sana. Madoa hapendi kusoma na anataka kusafiri Amerika. Wao si matajiri pia na Baba yake alifariki baada ya kuvamiwa na chui.

3) Mwamba si mtoto na anaweza kusema lugha zingi. Mwamba ni rafiki wa Madoa na atasaidia Madoa kwenda katika Amerika.

4) Mzee Zakayo Wekesa hawezi kusema Kiswahili kizuri. Alisikitika sana na alilia machozi na anafimbo na mzigo mkononi.

II. Pasipojulikana; nikamgeukia; akinionya; hata liwa liwalo; muzuri kitoko; itawaye; ninakudanganya; tulikuwa tukisoma.

III. Madoa ana ndoto nyingi ya Amerika na anataka kwenda. Isa na Madoa wote wanakaa na Mama zao na Baba zao walifariki. Wote wawili wanakaa katika kijiji cha Sangura. Madoa ni rafiki mkubwa wa Isa. Madoa anasema Mwamba atawasaidia kwenda Merekani. Hawapopendi kwao kwa sababu wao ni maskini na kawapendi shule. Madoa anataka Marekani kwa sababu anachukia kukaa kijijini Sangura sana sana. Lakini, sura ya kwanza inatuambia hajui yo yote juu ya Marekani.

Iqra Kamal said...

Sura ya Pili:

1) Isa yuko msituni kwa sababu alikimbia na nyumba kabla ya mama yake anaweza kumchapa viboko. Mama yake alikasirika na Isa kwa sababu madoa ana tabia mbaya, lakini Isa hasikii na ametembea naye tena na tena.

2) Katika ndoto ya Amerika ya Isa alikuwa kuendesha gari nyeusi kubwa sana na madoa walikuwa wako katika miji ya New York. Isa alikuwa akijifanya hakujui ambapo walikuwa na Madoa alikasirika, hasa wakati Isa alimuuliza kusoma maandishi inayoandikwa "New York". Madoa alifungua mlango huko gari linakwenda mbio na gurudumu moja likaruka kutoka gari wakati Isa akifunga breki. Madoa akabofya kifaa fulani kisha gurudumu likajirudisha. Isa aliona mabomba ya soda na vinywaji vingine ndani hoteli. Vyakula vinajipika na kujileta mezani. Aliona pia sahani zinajiosha na kujikausha na kitanda kijimletea alipotaka kulala.

3) Hapana, ndoto hiyo si ya kweli kwa sababu watoto kawaendeshi magari, vyakula havijipiki na havijileti, sahani hazijioshi na hazijikaushi, na vitanda havileti unapochoka.

5) Sura ya pili ni kuhusu Isa ana ndoto ya Amerika. Katka mwanzo yeye kamwe ana ndoto kuhusu Amerika lakni kuwa ni ndoto tu anataka. Aliamka asubuhi moja kulia na alimwambia mama yake hana ndoto ya Amerika kama Madoa ana. Mama yake alikasirika kwa sababu bado anatembea na Madoa. Wakati amemkaribia kumchapa alianguka na Isa aliendesha msituni wa Sangura. Isa alilala na ana ndoto ya Amerika chini ya mgunga mmoja mkubwa.