KARIBUNI TUJIFUNZE KISWAHILI - LUGHA NZURI NA RAHISI KUTOKA AFRIKA YA MASHARIKI. JISIKIE HURU KUTOA MAONI, KUULIZA NA KUJIBU MASWALI N.K. NI LAZIMA TUTUMIE LUGHA NZURI NA YA HESHIMA KWA KILA MTU. HAKUNA MATATA!
"Recipes" hizi ziliandaliwa na wanafunzi. Walipika vyakula hivi na kuvileta darasani na darasa lote lilivila na kujadiliana.
A. Mahitaji:
Mchele vikombe viwili
Maji vikombe sita
Nyama ya kuku kilo moja bila mifupa
Vitunguu saumu vitatu (three cloves)
Nyanya moja kubwa
Kitunguu kimoja kikubwa
Tangawizi
Masala ya biriyani vijiko vinne
Pilipili mbili
Pilipili hoho ya kutosha
Chumvi ya kutosha
Mafuta
B . Mchanganyiko:
Katakata kuku vipande vidogo halafu osha katika maji moto.
Changanya kitunguu saumu, pilipili, pilipili hoho, tangawizi, chumvi kijiko kimoja na mafuta robo kikombe katika “blender” na changanya mpaka iwe mchanganyiko mzuri sana.
Changanya mchanganyiko na kuku pamoja katika sufuria au “zip lock bag” na ni lazima“umarinate” kuku kwa masaa matatu au manne.
C. Biriyani:
Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo.
Washa moto na ongeza mafuta kwenye sufuria halafu kaanga kitunguu na nyanya vizuri sana.
Ongeza kuku na mchanganyiko katika sufuria.
Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
Osha mchele na maji moto, halafu baada ya kuosha ongeza mchele na maji vikombe sita katika sufuria
Ongeza chumvi ya kutosha na masala ya biriyani vijiko vinne.
Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
Kisha funika chakula na gazeti na kifuniko ili mvuke usitoke.
Wacha chakula kijipike kwa muda wa kama nusu saa hadi kimeiva.
Jibu maswali katika wimbo wa Mume Bwege. Majibu yako ni lazima yawe katika insha tafu fupi fupi zenye nusu ukurasa kila moja. Unaweza kuleta insha yako darasani Jumatatu au kuiweka katika blogu moja kwa moja kama maoni (comments)
Au
Andika insha ndefu (ukurasa mmoja na nusu) kuhusu makazi yako. Andika kila kitu kuanzia historia yako fupi - ulizaliwa wapi, nyumbani ni wapi, kama unapapenda, sasa unakaa wapi, kwa nini, unapenda kusafiri kwa njia gani, toa maelekezo ya watu kufika nyumbani kwako hapa Gainesville au nyumbani kwa wazazi wako. Hii ni insha ya jumla na lengo lake kuu ni kuhakikisha kwamba unajua kutoa na kufuata maelekezo (to give and follow directions). Be creative and try using any grammar that we have seen so far. Hapana shaghalabaghala!
Maneno yamewekwa hapa na darasa la Kiswahili la mwaka wa pili
Chuo Kikuu cha Florida, Gainesville
Nilikuwa na mpenzi wangu
Nani asiyemjua
Mtoto kaumbika
Utasema malaika
Miezi kadhaa ikasogea
Mtoto (wa) kwanza tukazaa
Mtoto katoka Mwarabu
Swali lilikosa jibu
Akasema we hujui
Mtoto kafata kwa babu
Nikagunaguna pale mzee nikauchuna
Mtoto (wa) pili tukazaa
Huyu wa sasa Mchina doh
Nikasema mama vipi
Mbona mi sielewi
Akasema we hujui
Huyu kafata kwa bibi
Aa wewe mama wee
Ingekuwa ungefanyeje
Mwenzenu nalala chini
Mke wangu kitandani
Nikilala kitandani
Kila mtu shuka lake
Mwenzenu nalala chini
Mke wangu kitandani
Nikilala kitandani
Basi ujue mzungu wa nne
Nikiuliza kwa nini
Anasema amenipa likizo eeh
Siyo kama napenda
Imenilazimu ooh
Siyo kama napenda
Ananilazimisha yoo
Mwenzenu naosha vyombo
Mwenzenu napiga deki
Mzee mzima napika
Jamani nafua nguo
Siyo kama napenda
Nalazimishwa mimi
Lo, hii sasa kali
Jana kaniambia anataka kwenda klabu na marafiki zake
Ila kaniambia mimi
Nilinde nyumba eti wezi wasije wakaiba
Eee Bize Man hii halali kweli
Oyaa Mbiye njoo unisaidie huku nyumbani mwenziyo naonewa
Chifu Rumanyika, unajifanya hujui
Ooo naonewa mimi
Aa wewe mama wee
Ingekuwa ungefanyeje
MSAMIATI
-jua - fahamu
umbika - naturally attractive
mzungu wa nne - opposite direction
likizo - mapumziko
lazimu - ni lazima
lazimisha- force to do something
osha - wash
vyombo - dishes
piga deki- kusafisha sakafu
fua nguo - wash clothes
linda - protect
wezi - wingi wa mwizi
iba - steal
halali - fair
onea - mistreat
=======================================
MASWALI:
Baada ya kutazama video hii na kusoma maneno ya wimbo huu:
(1) Andika tofauti za kitamaduni kati ya wanaume wa Kitanzania na wanaume wa Kimarekani. Ni lazima utumie kauli ya kutendea (prepositional form) mf. pika - pikia, soma - somea n.k.
Mfano: Kwa kawaida wanaume wa Kitanzania hawajipikii chakula lakini wanaume wa Kimarekani wakati mwingine wanajipikia chakula chao
(2) (Kwa wavulana/wanaume au jifanye (pretend) kuwa mwanaume), kama wewe ungekuwa ndiye unayeimbwa katika wimbo huu ungefanya nini?
Walimu ni watu muhimu sana katika maisha yetu. Wao hutufundisha kusoma, kuandika na kuwa na adabu nzuri. Lakini mara nyingi hawalipwi pesa nyingi, wanadharauliwa na wanafanya kazi katika mazingira magumu sana hasa kule Afrika.
Ungekuwa rais wa Tanzania, ungefanya nini kuwasaidia walimu kama huyu pichani anayemfundisha mtoto mdogo kuandika namba tano?
(1) Ufahamu na Insha: Someni na mfahamu kila kitu kuhusu sura ya kwanza na ya pili ya Ndoto ya Amerika. Kutakuwa na maswali mafupi ya insha kuhusu sura hizo mbili.
(2) Msamiati: Ni lazima mfahamu msamiati wote wa sehemu ambazo tumesoma na kutafsiri darasani. Utaweza kuulizwa kutafsiri, kutumia maneno ya msamiati katika sentensi au kuoanisha.
(3) Sarufi - Ni lazima ufahamu -have/has been, used to (past habitual) na past continuous tense (we were eating...) n.k.
Mtihani wa katikati utafanyika darasani siku ya Jumanne tarehe 26/2/2009. Mtihani utachukua saa moja na nusu. Topiki/mada za muhimu kuzingatia:
(1) Ni lazima uwe tayari kuandika insha fupifupi juu ya topiki zote ambazo tayari tumeshazisoma darasani mfano; kujistarehesha (somo la 8), Usafiri (somo la tisa), Kuwalea watoto (somo la 10), Hali ya Hewa (somo la 11) na kazi (somo la 12 - alama za ziada).
Kwa hivyo;
=> Utaulizwa maswali mafupi mfano - wewe unajistareheshaje? na utaandika insha fupi. Wewe sasa ni wmanafunzi wa mwaka wa pili na tunakutegemea kwamba unaweza kuandika insha nzuri na kujieleza kwa Kiswahili bila wasiwasi wo wote.
(2) Sarufi: Ni lazima ufahamu hu- tense negative, jinsi ya kufanya contractions, causative (sh-), conditional -ki- (positive na negative) na sarufi yote ambayo umeshasoma mpaka wakati huu. SITAKI ufanye makosa mabaya kabisa ya kisarufi kama vijana VYA, mji ya, mpenzi ya...Makosa kama haya yatakufanya upoteze pointi nyingi sana!
(3) Msamiati:Ni lazima ufahamu maneno yote kutoka zoezi la kusoma la somo la nane (Ninapenda sana kwenda ufukoni - uk 127-128) na zoezi la kusoma la somo la 10 (Malezi yangu - uk 151-152). Utaulizwa kuoanisha maneno (matching), kutafsiri pamoja na kutumia maneno hayo katika sentesi. Unaweza pia kuulizwa kutafsiri msamiati wo wote ambao tumeshaona darasani.
Huu utakuwa ni mtihani rahisi na hakuna shida ya kuwa na wasiwasi. Nitakuwa ofisini mwangu kesho Jumatano (25/2/2009) kuanzia saa sita mchana mpaka saa saba na nusu mchana. Unaweza kufika wakati huo kama una swali lolote. Unaweza pia kuniandikia e-mail kupitia profesamatondo@gmail.com. Nitakuwa nikitazama e-maili hii mara kwa mara.
(1) Usikilize tena wimbo wa Mtoto Akililia Wembe kutoka you tube aua hapa. Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja kuhusu swali lifuatalo '...mtoto akililia wembe tumpe?" Tumia causative angalau (at least) tano. (alama 20. Ninataka insha ndefu nzuri)
(2) Wewe ukiwa na watoto siku moja, utawapa adhabu gani ili kuwaadabisha? Utawapiga? Kwa nini? Andika jibu refu kuhusu suala hili. (alama 10)
(3) Fanya zoezi la tatu (ukurasa wa 154) katika kitabu chako. Kabla hujajibu swali hili, ni lazima kwanza utembelee hapa. (alama 13)
(4) Je, katika sikukuu hii ya Wapendanao utafanya nini? Andika insha fupi. (alama 10)
MUHIMU: Majibu ya swali la pili ni lazima yawekwe hapa kama maoni (comments). Majibu ya Maswali ya 1, 3 na 4 yaletwe darasani Jumanne ya wiki kesho (17/2/2009)
Tafuta mada yo yote kutoka katika magazeti, redio au kutoka sehemu yo yote na uwasilishe darasani kwa muda wa dakika tano hadi kumi. Tafadhali usisome na jaribu sana kutumia maneno yako mwenyewe.
(1) Tazama video ya MUME BWEGE (Stupid husband) hapo chini na soma maneno ya wimbo (lyrics) halafu jibu maswali (1) na (3). Majibu yako ni lazima yawe katika insha.
(2) Kuna chakula cho chote unachokipenda? Andika mahitaji ya chakula hicho na kinavyopikwa. Andika kila kitu ambacho unataka watu wengine wafahamu kuhusu chakula chako.
(3) Andika sentensi kumi ndefu ukitumia relative markers katika tense zifuatazo. Sentensi moja katika kila "tense" ni lazima iwe katika ukanushi (negative)
SWALI: Kuna chakula cho chote ambacho unaweza kula katika mkahawa huu wa "Sheraton"? Andika mazungumzo mafupi kati yako na mhudumu kuhusu jinsi utakavyohudumiwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho.