Wednesday, October 21, 2009

MAPISHI YA VYAKULA MBALIMBALI (RECIPES): BIRIYANI (NA PRIYA)

"Recipes" hizi ziliandaliwa na wanafunzi. Walipika vyakula hivi na kuvileta darasani na darasa lote lilivila na kujadiliana.
  • A. Mahitaji:
  1. Mchele vikombe viwili
  2. Maji vikombe sita
  3. Nyama ya kuku kilo moja bila mifupa
  4. Vitunguu saumu vitatu (three cloves)
  5. Nyanya moja kubwa
  6. Kitunguu kimoja kikubwa
  7. Tangawizi
  8. Masala ya biriyani vijiko vinne
  9. Pilipili mbili
  10. Pilipili hoho ya kutosha
  11. Chumvi ya kutosha
  12. Mafuta
  • B . Mchanganyiko:

  1. Katakata kuku vipande vidogo halafu osha katika maji moto.
  2. Changanya kitunguu saumu, pilipili, pilipili hoho, tangawizi, chumvi kijiko kimoja na mafuta robo kikombe katika “blender” na changanya mpaka iwe mchanganyiko mzuri sana.
  3. Changanya mchanganyiko na kuku pamoja katika sufuria au “zip lock bag” na ni lazima“umarinate” kuku kwa masaa matatu au manne.

  • C. Biriyani:

  1. Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo.
  2. Washa moto na ongeza mafuta kwenye sufuria halafu kaanga kitunguu na nyanya vizuri sana.
  3. Ongeza kuku na mchanganyiko katika sufuria.
  4. Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
  5. Osha mchele na maji moto, halafu baada ya kuosha ongeza mchele na maji vikombe sita katika sufuria
  6. Ongeza chumvi ya kutosha na masala ya biriyani vijiko vinne.
  7. Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
  8. Kisha funika chakula na gazeti na kifuniko ili mvuke usitoke.
  9. Wacha chakula kijipike kwa muda wa kama nusu saa hadi kimeiva.
  10. Epua na pakua baada ya kupoa.

No comments: