Monday, September 27, 2010

INSHA (ILETWE DARASANI JUMATANO - 29/10/2010)

  • Andika insha ndefu juu ya nyumba unayoitamani sana (your dream house). Andika kila kitu kuhusu nyumba hiyo. Since this is a hypothetical house, this is an excellent chance for you to practice -nge-, -ngeli- and -ngali- tense.

TOA MAELEZO MAFUPI YA JINSI YA KUFIKA KWAKO

  • Rafiki yako anataka kukutembelea na hajawahi kufika kwenu. Mpe maelezo marefu ya namna ya kufika kwenu kutokea Chuo Kikuu cha Florida kwa kutumia usafiri wa umma.

Monday, September 13, 2010

MISS TANZANIA 2010 - UNAWEZA KUSEMA LOLOTE?


Kwa habari zaidi soma hapa.

ZOEZI: TOA MAONI YAKO

I. Sikiliza wimbo huu hapa chini na kisha jibu maswali


    (a) Umeupenda wimbo huu? Kwa nini?

    (b) Unakubaliana na Dudu Baya kwamba "mwanamke tabia?" i.e Noeclexis

    II. Ungekuwa mtu mwenye nguvu kuliko wote na kiongozi wa taifa tajiri kuliko yote duniani mf. Rais wa Marekani ungefanya nini ili kusaidia watu masikini hapa Marekani na duniani kote.

    SARUFI YA -NGE- NA -NGA-; -NGALI- NA -NGELI - KUTOKA MWANASIMBA

    Tembelea hapa

    RATIBA YA KUWASILISHA DARASANI

    • Mada yoyote kutoka mahali popote.
    • HAKUNA kusoma - kuzungumza tu
    • Dakika tano - saba

    Septemba 2010

    Jumatano - Septemba 15 = Mary-A
    Ijumaa - Septemba 17 = Kelci D

    Jumatatu - Septemba 20 = Maria
    Jumatano - Septemba 22 = Taylor
    Ijumaa - Septemba 24 - Rachel G
    Jumatatu - Septemba 27 - Olivia
    Jumatano - Septemba 29 - Whitney

    Oktoba 2010

    Jumatatu - Oktoba 4 - Kayla V
    Jumatano - Oktoba 6 - Rachel GL
    Ijumaa - Oktoba 8 - Jenny M

    Wednesday, April 14, 2010

    EVALUATION CHANGES

    Mahudhurio ----10%

    Kushiriki/kuwasilisha ----10%

    Chemshabongo ----15%

    Kazi za nyumbani ----20%

    Kuwasilisha mradi wa muhula -----15%

    Mradi wa muhula ---20%

    Mtihani wa katikati ---10%


    Final project presentations (15 points)


    Each presentation will be 10 minutes long. Come prepared and don't waste any time. This is a chance for you to demonstrate your speaking skills by using the grammar that you know so far. You will NOT be allowed to read, even though it is OK for you to have guiding phrases/vocab. Use Renee's presentation as a model - simple, straightforward, using own words and just beautiful. The points will be distributed as follows:


    (1) Fluency - 3 pts


    (2) Grammar - 5 pts. Avoid the "obvious" grammatical mistakes. All agreement as well as tense and derivational mistakes will be penalized.


    (3) Cultural content and quality of the materials presented - 4 pts


    (4) General organization and aesthetics - 2 pts


    (5) Other - 1 pt.


    Final Projects (25 points)

    These are supposed to be SERIOUS projects that fully demonstrate your Swahili ability up to this point. That is why I stopped giving you quizzes and exams so that you can devote all your time and energy on them. I will grade them very keenly.

    Miradi yote (minimum 8 pages) iliyochapwa vyema ni lazima iletwe kwangu Jumatano tarehe 28/4/2010. Lete "hard copy" Grinter 325 kuanzia asubuhi mpaka saa 11 jioni. Pia tuma "attachment" kupitia profesamatondo@gmail.com. Katika project ninataka kuona mambo yafuatayo:

    (1) Uwezo wako wa kuandika Kiswahili sanifu (Standard Swahili)
    (2) Matumizi sanifu ya sarufi. You will lose points for "obvious" grammatical mistakes
    (3) Demonstrate your masterly of the grammar that we have seen in this year e.g. all the derivational morphemes like causatives, applicatives, passives, statives etc.
    (4) Mambo ya kitamaduni. You will be rewarded for bringing in cultural issues from both Shida and Ndoto ya Amerika. This will act as your extra credit!

    Important: Use pictures and diagrams only here and there. You should aim at 15 pages (with few diagrams). It will not help you to have 8 pages (double spaced with a lot of pictures + grammatical mistakes). This will simply not work!!!

    If you have any questions, let me know.

    ******************
    19/4 - Jumatatu

    Nikki
    Gloria
    Mackenzie
    Cheka
    Simba
    Elena

    21/4 - Jumatano

    Safina
    Nila
    Andrea
    Renee
    Jelani


    Wednesday, April 7, 2010

    SHIDA - SURA YA TANO na SITA

    Sura ya Tano - Maswali ya Majadiliano


    Ijumaa (9/4/2010)

    • Katika sura hii, Sefu yuko wapi? (Nila)
    • Shida alikutanaje tena na wazazi wake (uk 69 – 71)? (Nikki)
    • Sefu na Shida wameamua kurudi kijijini. Kwa nini? Isome vizuri barua ya Sefu aliyomwandikia abake (uk79 – 81) (Gloria na Dkt. Cheka)
    • Tazama tazama matarajio ya maisha bora kule vijijini (aya ya mwisho ukurasa wa 81 – 82). Ni kweli? (Jelani)
    • Sema kidogo juu ya ufupisho wa sura ya tano kwa maneno yako mwenyewe (Renee).


    Sura ya Sita - Maswali ya Majadiliano


    Wiki ijayo (Jumatatu na Jumatano)


    • Je, umeipenda riwaya ya Shida? Kwa nini? (Andrea)
    • Waswahili wana methali nyingi. Methali moja inasema kwamba “mchagua jembe si mkulima” . Je, unawezaje kutumia methali hii kueleza matatizo ya (Chonya) Sefu kama tulivyoona katika sura ya kwanza mpaka sura ya tatu ya riwaya ya SHIDA? (Safina)
    • Wahusika wakuu wa riwaya hii ni nani? Eleza machache juu ya tabia zao kwa kifupi. Ni yupi ambaye umempenda sana? Kwa nini? (Elena)
    • Eleza maisha ya Matika (Shida)? Je, yeye ni mfano halisi wa hali ya maisha ya wanawake wa Afrika? (Nikki)
    • Umejifunza nini kuhusu maisha ya watu katika Tanzania ya miaka ya sabini (na sasa) baada ya kusoma riwaya ya Shida? (Mwalimu)
    • Je, unaonaje kuhusu suluhisho la mwandishi? Je, kurudi vijijini kwa Chonya, Matika na Msafiri ndilo jibu sahihi kwa matatizo ya vijana na watu wengine wasio na kazi kule mijini? (Simba)

    KUWASILISHA MRADI WA MWISHO WA MUHULA NA MTIHANI WA MWISHO

    • Kuwasilisha ni dakika 10 - 15.
    • HAPANA kusoma! Tumia maneno yako mwenyewe na Kiswahili ambacho umeshajifunza mpaka sasa. Unaweza kutayarisha "powerpoint"

    19/4 - Jumatatu

    Nikki
    Gloria
    Mackenzie
    Cheka
    Simba
    Elena

    21/4 - Jumatano

    Safina
    Nila
    Andrea
    Renee
    Jelani

    Miradi yote iliyochapwa vyema ni lazima iletwe kwangu Jumatano tarehe 28/4/2010

    *******************
    MTIHANI WA MWISHO
    **********************

    Utafanyika darasani: Jumatatu - 26/4/2010 saa 9 - 11 jioni (3 PM - 5 PM)


    MWISHO WA KUWASILISHA MAKALA DARASANI

    9/4 (Ijumaa) - Andrea
    12/4 (Jumatatu) - Renee
    14/4 (Jumatano) - Nila

    Thursday, February 25, 2010

    MIDTERM KESHO

    • The Midterm will be a short exam (50 min). It will cover the following topics.
    1. Shida - chapters (1) and (2). Make sure you can answer the questions in your guiding handout.
    2. You will write at least one short essay.
    3. There will be a section where you will be required to correct ungrammatical Swahili sentences. This will be a collection of mistakes that you make during your daily presentations. We always correct them together.
    4. Vocabulary - you will be asked to use certain words/phrases in a sentence (e.g. -starehesha, shukrani ya punda etc).
    5. Sarufi - you must understand how the stative marker (http://mwanasimba.online.fr/E_Chap41.htm) and class 15 noun class - ku (http://mwanasimba.online.fr/E_Chap03.htm)
    6. This also means that I can ask you anything I assume that you MUST know at this stage e.g. anything that was covered in Hinnebusch and last semester (e.g. passives, http://mwanasimba.online.fr/E_Chap37.htm- applicatives -http://mwanasimba.online.fr/E_Chap38.htm etc).

    Friday, February 5, 2010

    ZOEZI LA PILI LA KUANDIKA - JUMATATU (8/2/2010)

    • Andika ufupisho wa sura ya kwanza ya Shida.
    • Andika jinsi Matika alivyoondoka kwenda mjini na jinsi alivyorudi. Tunajifunza nini kuhusu maisha ya vijijini na mijini kwa kumwangalia Matika alivyoondoka na alivyorudi? TUMIA MANENO YAKO MWENYEWE!
    • Tumia maneno yafuatayo katika sentensi:
    1. mpiga debe
    2. -vunja ungo
    3. siri
    4. kindakindaki

    RATIBA YA KUWASILISHA MADA DARASANI - KILA SIKU

    MWEZI WA PILI (Dk. 5 - 10)

    8/2 - Jelani
    10/2 - Nikki
    12/2 - Gloria
    15/2 - Mackenzie
    17/2 - Cheka
    19/2 - Simba
    22/2 - Elena
    24/2 - Safina
    26/2 - Nila

    MWEZI WA TATU (Dk. 5 - 10)

    1/3 - Andrea
    3/3 - Renee
    5/3 - Jelani

    Wednesday, October 21, 2009

    SOMO LA SITA (VYAKULA NA MAPISHI)

    Baada ya somo hili ni lazima:

    (1) Ufahamu kuagiza chakula katika mahoteli na mikahawa utakapotembelea Afrika Mashariki

    (2) Kutoa maelekezo na kupika angalau chakula kimoja cha Afrika Mashariki

    => Soma maelezo ya jinsi ya kupika pilau (uk. 103). Fanya zoezi linalofuatia.

    => Chagua chakula kimoja cha Kimarekani au Kiafrika na uelezee mahitaji na hatua za kufuata wakati wa kukiandaaa.

    => Fanya zoezi la Kumi na moja (Zoezi la Kusoma na Kuandika uk 104-105).

    Methali: Pilipili usiyoila, yakuwashia nini?

    Kitanza ulimi: (1) Wali wa liwali huliwa na wanawali, wasio wanawali hawali wali
    (2) Waacheni wali wale wale wali wao

    MAPISHI YA VYAKULA MBALIMBALI (RECIPES): BISKUTI YA CHOKOLETI (NA KYLIE)

    Mahitaji:

    -Unga wa ngano vikombe viwili

    -Hamira kijiko cha chai moja

    -Chumvi kijiko cha chai moja

    -Siagi vikombe moja

    -Sukari vikombe moja

    -Sukari hadharani vikombe nusu

    -Mayai makubwa mawili

    -Chokoleti vikombe viwili


    Kuandaa Biskuti na Chokoleti:


    -Uchemshe jiko katika 190C

    -Uongoze unga wa ngano, hamira, na chumvi katika bakuli

    -Halafu uongoze siagi, sukari, sukari hadharani, na mayai katika bakuli nyingine na changanya

    -Uongoze bakuli la kwanza katika bakuli la pili na changaya

    -Uchanganye chokoleti na kila kitu

    -Uweke mchanganyiko katika chombo

    -Oka kwa dakika kumi na tano

    -Halafu kula

    MAPISHI YA VYAKULA MBALIMBALI (RECIPES): BIRIYANI (NA PRIYA)

    "Recipes" hizi ziliandaliwa na wanafunzi. Walipika vyakula hivi na kuvileta darasani na darasa lote lilivila na kujadiliana.
    • A. Mahitaji:
    1. Mchele vikombe viwili
    2. Maji vikombe sita
    3. Nyama ya kuku kilo moja bila mifupa
    4. Vitunguu saumu vitatu (three cloves)
    5. Nyanya moja kubwa
    6. Kitunguu kimoja kikubwa
    7. Tangawizi
    8. Masala ya biriyani vijiko vinne
    9. Pilipili mbili
    10. Pilipili hoho ya kutosha
    11. Chumvi ya kutosha
    12. Mafuta
    • B . Mchanganyiko:

    1. Katakata kuku vipande vidogo halafu osha katika maji moto.
    2. Changanya kitunguu saumu, pilipili, pilipili hoho, tangawizi, chumvi kijiko kimoja na mafuta robo kikombe katika “blender” na changanya mpaka iwe mchanganyiko mzuri sana.
    3. Changanya mchanganyiko na kuku pamoja katika sufuria au “zip lock bag” na ni lazima“umarinate” kuku kwa masaa matatu au manne.

    • C. Biriyani:

    1. Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo.
    2. Washa moto na ongeza mafuta kwenye sufuria halafu kaanga kitunguu na nyanya vizuri sana.
    3. Ongeza kuku na mchanganyiko katika sufuria.
    4. Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
    5. Osha mchele na maji moto, halafu baada ya kuosha ongeza mchele na maji vikombe sita katika sufuria
    6. Ongeza chumvi ya kutosha na masala ya biriyani vijiko vinne.
    7. Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
    8. Kisha funika chakula na gazeti na kifuniko ili mvuke usitoke.
    9. Wacha chakula kijipike kwa muda wa kama nusu saa hadi kimeiva.
    10. Epua na pakua baada ya kupoa.