Showing posts with label MAZOEZI. Show all posts
Showing posts with label MAZOEZI. Show all posts

Monday, April 9, 2012

ZOEZI LA LEO - WEKA MAJIBU YAKO HAPA KAMA MAONI


Shida Sura ya Tano - Uk. 11 katika Mwongozo wa Shida

(1) Katika sura hii Sefu yuko wapi? Kwa nini?

(2) Sefu na Shida wameamua kurudi kijijini. Kwa nini? Isome vizuri barua ya Sefu aliyomwandikia Babake (uk. 79-81)

Monday, November 21, 2011

FANYA ZOEZI HILI SIKU YA JUMATANO - WEKA MAJIBU YAKO KAMA KOMENTI/MAONI

Kama ndoto ya Issa inavyoonyesha, watu wengi hufikiri kwamba maisha ya Amerika ni maisha ya raha mustarehe. Sasa rafiki yako mliyekutana naye Afrika anakutaka umsaidie kuja Marekani. Yeye anafikiri kwamba akija Marekani atapata maisha mazuri sana - kazi nzuri, pesa nyingi, magari ghali na raha nyinginezo. Mwandikie barua NDEFU ukimweleza ukweli kuhusu maisha ya Marekani na ungetaka afanye nini. Yeye sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Yeye anasomea ualimu.

Wednesday, September 21, 2011

Zoezi la Kwanza: Fall 2011

Soma Sarufi ya Somo la Pili

 (1) Every and each (kila) - uk. wa 35, (2) The relative constructions (uk.36) and (3) the -o construction (uk.37)

Fanya Zoezi la Tatu: Maswali ya Kisarufi (uK.39). Andika majibu yako hapa chini kama maoni (comments)

Monday, April 4, 2011

LEO NI TAREHE 4/4/2011 - ZUNGUMZENI JUU YA MASWALI HAYA

Important

Remain in the classroom. Discuss the questions below in two groups. Towards the end of the class, spare about 10 minutes and write your answers as comments on this post. The answers don't have to be too long. I just want to see what you think. Please, write your names.

*****************
Shida Sura ya Nne
  • Sefu anakutana na Shida katika baa ya Starehe (ukurasa wa 62 aya ya mwisho). Shida alikuwa anafanya kazi gani? Unaipenda kazi yake. Kwa nini? = Jibu swali hili.
  • Sefu na Shida walisameheana na kuendelea na mapenzi yao. Sasa Jifanye (Now pretend). Kama wewe ungekuwa Sefu ungefanyeje? Ungemsamehe Shida? = Jibu swali hili.
  • Shida anapata mimba (ukurasa wa 63 aya ya mwisho) na anahamia kwa Sefu (ukurasa wa 64 aya ya pili na kuendelea)
  • Sefu anaanza kufanya kazi mpya (ukurasa wa 66 aya ya nne …Lala masikini, amka tajiri…. Soma mpaka mwisho wa sura). Ni kazi gani? Unaipenda? = Jibu swali hili.
  •  Andika ufupisho wa sura hii kwa kutumia maneno yako mwenyewe. = Jibu swali hili (kama kuna muda)

Friday, March 25, 2011

ZOEZI LA NYUMBANI

  • Andika ufupisho wa Shida aya ya tatu kwa maneno yako mwenyewe! (Ukurasa 1)
  • Andika sentensi tano kwa kutumia stative marker.

Majibu yote yawekwe hapa hapa kwenye blogu

Monday, September 13, 2010

ZOEZI: TOA MAONI YAKO

I. Sikiliza wimbo huu hapa chini na kisha jibu maswali


    (a) Umeupenda wimbo huu? Kwa nini?

    (b) Unakubaliana na Dudu Baya kwamba "mwanamke tabia?" i.e Noeclexis

    II. Ungekuwa mtu mwenye nguvu kuliko wote na kiongozi wa taifa tajiri kuliko yote duniani mf. Rais wa Marekani ungefanya nini ili kusaidia watu masikini hapa Marekani na duniani kote.