Wednesday, October 21, 2009
SOMO LA SITA (VYAKULA NA MAPISHI)
(1) Ufahamu kuagiza chakula katika mahoteli na mikahawa utakapotembelea Afrika Mashariki
(2) Kutoa maelekezo na kupika angalau chakula kimoja cha Afrika Mashariki
=> Soma maelezo ya jinsi ya kupika pilau (uk. 103). Fanya zoezi linalofuatia.
=> Chagua chakula kimoja cha Kimarekani au Kiafrika na uelezee mahitaji na hatua za kufuata wakati wa kukiandaaa.
=> Fanya zoezi la Kumi na moja (Zoezi la Kusoma na Kuandika uk 104-105).
Methali: Pilipili usiyoila, yakuwashia nini?
Kitanza ulimi: (1) Wali wa liwali huliwa na wanawali, wasio wanawali hawali wali
(2) Waacheni wali wale wale wali wao
MAPISHI YA VYAKULA MBALIMBALI (RECIPES): BISKUTI YA CHOKOLETI (NA KYLIE)
-Unga wa ngano vikombe viwili
-Hamira kijiko cha chai moja
-Chumvi kijiko cha chai moja
-Siagi vikombe moja
-Sukari vikombe moja
-Sukari hadharani vikombe nusu
-Mayai makubwa mawili
-Chokoleti vikombe viwili
Kuandaa Biskuti na Chokoleti:
-Uchemshe jiko katika 190C
-Uongoze unga wa ngano, hamira, na chumvi katika bakuli
-Halafu uongoze siagi, sukari, sukari hadharani, na mayai katika bakuli nyingine na changanya
-Uongoze bakuli la kwanza katika bakuli la pili na changaya
-Uchanganye chokoleti na kila kitu
-Uweke mchanganyiko katika chombo
-Oka kwa dakika kumi na tano
-Halafu kula
MAPISHI YA VYAKULA MBALIMBALI (RECIPES): BIRIYANI (NA PRIYA)
- A. Mahitaji:
- Mchele vikombe viwili
- Maji vikombe sita
- Nyama ya kuku kilo moja bila mifupa
- Vitunguu saumu vitatu (three cloves)
- Nyanya moja kubwa
- Kitunguu kimoja kikubwa
- Tangawizi
- Masala ya biriyani vijiko vinne
- Pilipili mbili
- Pilipili hoho ya kutosha
- Chumvi ya kutosha
- Mafuta
- B . Mchanganyiko:
- Katakata kuku vipande vidogo halafu osha katika maji moto.
- Changanya kitunguu saumu, pilipili, pilipili hoho, tangawizi, chumvi kijiko kimoja na mafuta robo kikombe katika “blender” na changanya mpaka iwe mchanganyiko mzuri sana.
- Changanya mchanganyiko na kuku pamoja katika sufuria au “zip lock bag” na ni lazima“umarinate” kuku kwa masaa matatu au manne.
- C. Biriyani:
- Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo.
- Washa moto na ongeza mafuta kwenye sufuria halafu kaanga kitunguu na nyanya vizuri sana.
- Ongeza kuku na mchanganyiko katika sufuria.
- Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
- Osha mchele na maji moto, halafu baada ya kuosha ongeza mchele na maji vikombe sita katika sufuria
- Ongeza chumvi ya kutosha na masala ya biriyani vijiko vinne.
- Changanya vitu hivi vyote kwenye sufuria vizuri sana.
- Kisha funika chakula na gazeti na kifuniko ili mvuke usitoke.
- Wacha chakula kijipike kwa muda wa kama nusu saa hadi kimeiva.
- Epua na pakua baada ya kupoa.
Tuesday, October 20, 2009
TOVUTI JUU YA MAGONJWA MBALIMBALI
Monday, October 19, 2009
Friday, October 9, 2009
INSHA YA TATU - ILETWE DARASANI JUMATATU (12/10/2009)
Au
Wednesday, October 7, 2009
MUME BWEGE (NA BUSHOKE - MWANAMUZIKI WA BONGO FLEVA KUTOKA TANZANIA)
Tazama video hii na soma maneno ya wimbo (lyrics)
MUME BWEGE (NA BUSHOKE – TANZANIA)
Maneno yamewekwa hapa na darasa la Kiswahili la mwaka wa pili
Chuo Kikuu cha Florida, Gainesville
Nilikuwa na mpenzi wangu
Nani asiyemjua
Mtoto kaumbika
Utasema malaika
Miezi kadhaa ikasogea
Mtoto (wa) kwanza tukazaa
Mtoto katoka Mwarabu
Swali lilikosa jibu
Akasema we hujui
Mtoto kafata kwa babu
Nikagunaguna pale mzee nikauchuna
Mtoto (wa) pili tukazaa
Huyu wa sasa Mchina doh
Nikasema mama vipi
Mbona mi sielewi
Akasema we hujui
Huyu kafata kwa bibi
Aa wewe mama wee
Ingekuwa ungefanyeje
Mwenzenu nalala chini
Mke wangu kitandani
Nikilala kitandani
Kila mtu shuka lake
Mwenzenu nalala chini
Mke wangu kitandani
Nikilala kitandani
Basi ujue mzungu wa nne
Nikiuliza kwa nini
Anasema amenipa likizo eeh
Siyo kama napenda
Imenilazimu ooh
Siyo kama napenda
Ananilazimisha yoo
Mwenzenu naosha vyombo
Mwenzenu napiga deki
Mzee mzima napika
Jamani nafua nguo
Siyo kama napenda
Nalazimishwa mimi
Lo, hii sasa kali
Jana kaniambia anataka kwenda klabu na marafiki zake
Ila kaniambia mimi
Nilinde nyumba eti wezi wasije wakaiba
Eee Bize Man hii halali kweli
Oyaa Mbiye njoo unisaidie huku nyumbani mwenziyo naonewa
Chifu Rumanyika, unajifanya hujui
Ooo naonewa mimi
Aa wewe mama wee
Ingekuwa ungefanyeje
MSAMIATI
-jua - fahamu
umbika - naturally attractive
mzungu wa nne - opposite direction
likizo - mapumziko
lazimu - ni lazima
lazimisha - force to do something
osha - wash
vyombo - dishes
piga deki - kusafisha sakafu
fua nguo - wash clothes
linda - protect
wezi - wingi wa mwizi
iba - steal
halali - fair
onea - mistreat
Baada ya kutazama video hii na kusoma maneno ya wimbo huu:
(1) Andika tofauti za kitamaduni kati ya wanaume wa Kitanzania na wanaume wa Kimarekani. Ni lazima utumie kauli ya kutendea (prepositional form) mf. pika - pikia, soma - somea n.k.
Mfano: Kwa kawaida wanaume wa Kitanzania hawajipikii chakula lakini wanaume wa Kimarekani wakati mwingine wanajipikia chakula chao
(2) (Kwa wavulana/wanaume au jifanye (pretend) kuwa mwanaume), kama wewe ungekuwa ndiye unayeimbwa katika wimbo huu ungefanya nini?
(3) Umeupenda wimbo huu? Kwa nini?
Friday, September 11, 2009
MAZOEZI YA -NGE-, -NGALI- NA -NGELI-
(1) Barack Obama -Raisi wa arobaini na nne wa Marekani
(2) Rush Limbaugh - Mtangazaji wa redio ya kihafidhina
(3) Machen - Rais wa chuo Kikuu cha Florida
(4) George Bush - Rais wa arobaini na tatu wa Marekani
(5) Wewe - kuna kitu cho chote ambacho unafikiri kwamba ni afadhali usingekifanya?