Monday, September 22, 2008

SOMO LA TATU - MIJI YA AFRIKA YA MASHARIKI

(1) Soma monolojia na jaribu kujibu maswali ya ufahamu (comprehension)

(2) Fanya zoezi la pili (uk 53)

(3) Soma habari za Sarufi na fanya mazoezi yanayofuatia.

(4) Fanya zoezi la Nne (uk 56-57)

(5) Fanya zoezi la Nane (uk 61)

(6) Soma habari za kitamaduni

(7) Angalia msamiati mwishoni

Wednesday, September 17, 2008

MASHAMBULIZI YA BOMU YEMEN (MADA YA HUGH)

Jana magaidi waliushambulia ubalozi wa Marekani nchini Yemen kwa bomu la gari na watu zaidi ya kumi wamefariki. Inasemekana magaidi wa Islamic Jihad au Al Qaida ndiyo wamefanya shambulizi hilo. Katika kufanya shambulizi hilo, magaidi walijifanya kuwa polisi wa Yemen. Rais George Bush wa Marekani amesema Marekani haitatishwa na magaidi na aliwaita kuwa ni waoga.
===============
Sasa jaribu kujibu maswali haya:

(1) Magaidi ni watu gani? Wewe unawapenda? Kwa nini?


(2) Wewe ungekuwa rais wa Marekani ungefanya nini kupambana na
magaidi na ugaidi?


(3) Toa maana za maneno yafuatayo:

Wanamgambo, ubalozi

(4) Kuna tofauti gani kati ya kufa na kufariki?


(5) Kujifanya ni nini? Wakati wa Haloween wewe hupenda kujifanya kuwa nani?

Monday, September 15, 2008

RATIBA YA KUWASILISHA MADA DARASANI

(1) Chagua mada yo yote
(2) Jiandae vizuri
(3) Wasilisha mada darasani (kuzungumza tu hakuna kusoma) - dakika 5 - 10
(4) Wasikilizaji watauliza maswali.

Hii ni sehemu ya kushiriki kwako (Participation)

Jumatano (9/17) - Hugh

Ijumaa (9/19) - Joy

Jumatatu (9/22) - Lydia

Jumatano (9/24) - Traci

Jumatatu (9/29) - Ashley

WHAT HAPPENS IN LAS VEGAS STAYS IN LAS VEGAS!

TANZANIA BILA UKIMWI

Wednesday, September 10, 2008

KAZI YA LEO NA IJUMAA

Andika insha ndefu nzuri (si chini ya ukurasa mmoja) juu ya mtu ambaye ungetaka kuwa au kitu ambacho ungependa kukifanya siku moja. Leta insha yako siku ya Ijumaa na tutazungumza juu ya insha nne hivi kabla ya kufanya chemshabongo ya kwanza.

Chemshabongo ya kwanza itakuwa juu ya -nge- na haiba za watu (personalities) . Someni notisi zenu za darasani na mfahamu kila kitu.

Leo mmenifurahisha jinsi mlivyozungumza darasani. Safi sana!

MARAISI WA TANZANIA

MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Raisi wa kwanza. Alikuwa raisi mwadilifu aliyeipenda sana Tanzania na watu wake. Hakuwa fisadi wala mla rushwa. Wakati wake watoto wote tulisoma bure na huduma za afya zilikuwa bure pia. Ningependa kuwa kama yeye kama ningekuwa raisi wa Tanzania.



















NDUGU ALI HASSAN MWINYI
Raisi wa pili. Yeye alikuwa raisi mpole na legelege. Rushwa na ufisaidi vilistawi sana katika kipindi chake. Yeye aliitwa Mzee Rukhsa kwa tabia yake ya kusema ndiyo kwa kila kitu hata katika mambo ya rushwa. Nisingependa kuwa kama yeye kama ningekuwa raisi wa Tanzania
















MHESHIMIWA BENJAMIN MKAPA
Raisi wa tatu. Yeye ni mwanafunzi wa Mwalimu Nyerere na Nyerere alimchagua. Nyerere pengine hakumjua vizuri mwanafunzi wake kwa sababu raisi huyu anasemwasemwa kwamba alikuwa fisadi na mla rushwa. Kama ni kweli basi yeye ni raisi mbaya. Mwalimu Nyerere angekuwa hai ningemwuliza kwanini alituchagulia raisi mbaya kama huyu. Nisingependa kuwa Ben. Mkapa kama ningekuwa raisi wa Tanzania leo.
















JAKAYA KIKWETE
Raisi wa nne. Yeye ni raisi kijana na mwenye bashasha na anapendwa na watu. Kila alipohutubia alisema "Maisha bora kwa kila Mtanzania" na Watanzania wengi walimwamini. Ni miaka karibu mitatu sasa na hakuna maisha bora kwa kila Mtanzania. Ijapokuwa yeye si fisadi lakini serikali yake imeshindwa kabisa kupambana na ufisadi na rushwa ya waziwazi. Yeye ameanza vibaya lakini ngoja tuone atakavyoendelea na utawala wake. Ninampenda.



















SWALI: Ni raisi gani wa Marekani unayempenda sana? Kwa nini? Na yupi ambaye humpendi sana? Kwa nini?

Monday, September 8, 2008

UJUMBE WA KANGA

Kanga hii inatoa ujumbe gani? Unakubaliana na ujumbe huo?

UFISADI

Fisadi ni nani? Wewe unapenda ufisadi?

KIPANYA NA SAFARI YA RAIS BUSH TANZANIA

Katuni hii inaeleza nini?

MWANASIASA

Wanasiasa ni watu wa aina gani? Chagua mwanasiasa mmoja na uzungumze kidogo juu yake. Unampenda? Kwa nini?



Friday, September 5, 2008

THE -NGE- TENSE

Tembeleeni http://mwanasimba.online.fr/E_Chap47.htm na kusoma kila kitu kuhusu matumizi ya -nge- tense. Tutazungumza juu ya "tense" hii Jumatatu.