Wednesday, October 20, 2010

NDOTO YA AMERIKA - PATA KOPI YAKO SASA


Nenda hapa na chapisha (print) kitabu chote cha ndoto ya Amerika (kurasa 48). Anza kusoma sura ya kwanza mara moja. Nitaweza mwongozo hapa baadaye.

MDUDU HATARI KULIKO WOTE DUNIANI

Mdudu huyu anaitwaje? Kwa nini unafikiri kwamba yeye ndiye mdudu hatari kabisa kuliko wote hapa duniani?

DAWA ZA KIENYEJI














Dr. Nkungu - mganga wa kienyeji











Dr. Mantori - mganga wa kienyeji













Wamasai wanauza dawa za kienyeji barabarani

HARUSI YA MARIAMU

(II) Harusi ya Mariamu: Ninapenda majibu marefu. Tafadhali usitoe majibu mafupi au ambayo si kamili.

(1) Umeipenda filamu hii? Kwa nini? Filamu ni juu ya nini?

(2) Ni arusi ya aina gani inayoonyeshwa katika filamu hii?

(3) Mariamu alikuwa anaumwa nini? Nini kiini cha ugonjwa wake? Kwa nini madaktari walishindwa kugundua ugonjwa wo wote?

(4) Kuna tofauti zo zote kati ya waganga wa kienyeji na madaktari katika hospitali za kisasa? Je, kuna waganga hapa Marekani? Kama wapo wanatibu magonjwa gani?

(5) Una maoni gani kuhusu waganga wa kienyeji? Unawapenda? Kwa nini?

(5) Tumia maneno haya katika sentensi:

-nakuhakikishia
-pona
-pasa

II. Andika maana, dalili, kinga na matibabu ya ugonjwa mmoja wa kawaida hapa Marekani.

Monday, October 4, 2010

SAHIHISHA MAKOSA - CORRECT THE MISTAKES

Ninafikiri yeye ni nzuri na gauni yake ni nzuri, pia

Napenda gauni nyekundu yake!

Mwanamke Tanzania hii ni mrembo sana na mrefu

Ufahamu yangu kwa utamaduni ya TZ (kijiji) ni kwamba si safi kuonyesha au kufununua mwili ya mtu sana

Mshindi, ana mrefu na ana kifahari. Ana furaha kwa sababu anakushinda the crown na motokaa. Atakushindana katika Miss Universe?

Ninapenda hizi. Miguu yake ni mizuri,na kuwa na magari yake ni safi.

Ninataka nina miguu kama yake!

Ningefurahi sana kukutana Miss Tanzania kwa sababu yeye ni nzuri sana sana!

Kuna sehemu ya utamaduni ya Amerika kwamba sipendi

Pia, ni lazima ajibu maswali na akili ili majaji wanajua utu uke

Chanzo (source): Click here.

CHEMSHABONGO YA TATU - KUFANYIA NYUMBANI (ILETWE DARASANI IJUMAA)

(1) Fanya swali la kwanza la zoezi la pili (uk 53)

(2) Soma habari za Sarufi na fanya mazoezi yanayofuatia (uk. 55).

(3) Fanya zoezi la Nne (uk 56-57)

(4) Fanya swali la kwanza kutoka zoezi la Nane (uk 61)

(5) Watoto hawa ni lazima waende shule na baba ana pikipiki moja tu na hana gari. Je, ungekuwa wewe ungefanya nini?


SOMO LA NNE - KUUZA NA KUNUNUA

(1) Someni habari za Sarufi (uk. 69-70)



(2) Someni mazungumzo ya pili (uk. 73 - 75) na hakikisheni kwamba mnafahamu maneno yaliyokolezwa (bolded). Mkazo (attention) pia ni katika vitenzi ambatano (compound verbs) m.f. -tunamtaka atuambie, tunataka kwenda, tutakuona utakapokuja, tulimwona alipokinunua, nilikuna ninakula n.k.



(3) Ni lazima msome mazoezi ya UTAMADUNI (uk. 77)



(4) Ni lazima mfahamu jinsi ya kununua vitu kwa wauzaji wadogo wadogo na jinsi ya kuomba punguzo la bei.